1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wulff kuwania urais wa Ujerumani

4 Juni 2010

Muungano unaoongoza serikali nchini Ujerumani, wa mrengo wa kati kulia, wa Kansela Angela Merkel umemteua waziri mkuu wa jimbo la Lower Saxony Christian Wulff kuwa mgombea wa kiti cha urais.

https://p.dw.com/p/Nhk6
Mgombea urais wa Ujerumani kutoka muungano wa chama tawala Christian Wulff kulia akiwa na Kansela Angela MerkelPicha: AP

Akitangaza uamuzi huo, Kansela Merkel amesema Wulff mwenye umri wa miaka 50 ni mtu mbunifu, ambaye anaweza kuisaidia nchi kimawazo.

Vyama vya upinzani vya SPD na kile cha kijani vimemchagua mwanaharakati wa iliyokuwa Ujerumani mashariki Joachim Gauck kuwa mgombea wake.

Hata hivyo mgombea kutoka katika muungano wa bibi Merkel, Christian Wulff anaelekea kushinda nafasi hiyo, kutokana na muungano huo, kuwa na wabunge wengi katika baraza la wawakilishi ambalo ndio linachagua Rais.

Ujerumani inahitaji Rais mpya kushika nafasi ya Horst Köhler, ambaye alijiuzulu bila ya kutegemewa mwanzoni mwa wiki.

Mwandishi:Halima Nyanza

Mhariri:Aboubakary Liongo