1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wydad Casablanca mabingwa CAF Super Cup

26 Februari 2018

Wydad Casablanca sasa ndio mabingwa wa Super Cup ya shirikisho la soka barani Afrika CAF.

https://p.dw.com/p/2tMju
CAF Champions League Al-Ahly - Wydad Casablanca
Picha: Getty Images/AFP/F. Senna

Kombe hilo linawapatanisha bingwa wa ligi ya vilabu bingwa Afrika na bingwa wa kombe la mashirikisho Afrika.

Wydad ambao ndio mabingwa wa Ligi ya Vilabu bingwa walikuwa wanacheza Jumamosi na TP Mazembe ambao ndio washindi wa kombe la mashirikisho na wakaebuka kidedea moja bila Amin Tighazoui akiwa mfungaji wa goli hilo la pekee katika dakika ya 83 mjini Casablanca.

Ule mfumo wa kumsaidia muamuzi kupitia video ulitumiwa kwa mara ya kwanza Afrika katika mechi hiyo baada ya kutumiwa katika ligi kadhaa Ulaya na kutoa matokeo tofauti tofauti.

Mwandishi: Jacob Safari/DPAE/Reuters

Mhariri: Josephat Charo