1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yaliyoandikwa na wahariri wa Ujerumani hii leo

22 Novemba 2006

Matumizi ya nguvu shuleni na mwaka mmoja wa serikali kuu

https://p.dw.com/p/CHUO

Kisa cha kuvamiwa shule katika mji wa Emsdetten huko Münster na jinsi michezo ya Computor inavyowakoroga akili watoto na pia mwaka mmoja tangu serikali ya muungano wa vyama vikuu ilipoingia madarakani,ndizo mada zilizochambuliwa na wahariri wa magazeti ya ujerumani hii leo.

Baada ya kisa cha yule mwanafunzi aliyekua na umri wa miaka 18 ,Sebastian B kuivamia shule yake ya zamani huko Emsdetten na kuwajeruhi watu zaidi ya 30,wanasiasa kwa mara nyengine tena wanataka ipigwe marufuku michezo ya computor inayoonyesha matumizi ya nguvu ,mfano “Counter Strike”.Idadi kubwa ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani wanakosoa lakini hoja hizo.

Gazeti la Frankfurter Allgemeine linaandika:

„Inakwenda kwendaje hata mtoto aliyekua hodari,aliyefika hadi ya kusifiwa na baadhi ya watu kama mwenye kipaji,akaja kubadilika na kua kitisho kwa jamii?Bila ya shaka sio pekee kutokana na michezo ya Computor .Ingawa michezo kama hiyo inaweza kumfanya mtu afikirie mambo ya kiajabu ajabu na matumizi ya nguvu,lakini pia inaweza kumfanya amlaani shetani.Kwanini maafisa wa idara za serikali hawajagutuka tangu walipogundua kwamba Sebastian B. anamiliki silaha bila ya kibali?Pasingehitajika makubwa kutambua kwamba pengine Sebastian angejiona amekabwa kwa kushtakiwa mahakamani,sawa na yaliyomtokea wakati mmoja Robert Steinhäuser.

Gazeti la WESTDEUTSCHEN la mjini Düsseldorf linaandika:

„Marufuku ya michezo ya computor inayoonyesha mauwaji hayatazuwia visa vya umwagaji damu kama ilivyoshuhudiwa mjini Erfurt au Emsdetten.Na zaidi ya hayo kuna mtandao wa Internet ambao vijana wanautumia pia kupata majina ya michezo waitakayo.Hatua za aina nyengine ndio zinazohitajika:Kwa mfano,baada ya kisa cha Erfurt,kila shule ingepatiwa mtaalam wa saikolojia..Bila ya kuwepo mtaalam kama huyo katika shule ,itakua vigumu kuwatambua na kuwashughulikia mapema watoto wanaojikuta katika hatari ya kuchanganyikiwa.Zaidi ya hayo watoto wanaofanya visa kama hivyo mara nyingi wanakua wakizungumzia wakifikiricho-lakini hakuna anaeamini wakisemacho.Inamaanisha siku za mbele watu wasidharau kisemwacho.

Gazeti la TRIERISCHE VOLKSFREUND linajishughulisha zaidi na silaha alizokua nazo Sebastian B .Gazeti linaandika:

„Robert Steinhäuser,aliyewauwa watu 16 kabla ya kujiuwa mwenyewe mwaka 2002 katika shule ya sekondari ya Gutenberg-Gymnasium mjini Erfurt,na kijana wa miaka 18 aliyewajeruhi watu 31 na kujiuwa baadae huko Emsdetten,hawakuhitaji Joysticks.Sebastian B alikua na bunduki nne.Amezipata wapi?Atakaelichunguza na kulipatia jibu suala hilo,atakua na nafasi nzuri ya kuzuwia visa kama hivyo visitokee tena humu nchini.

Mada ya ili magazetini inahusu serikali ya muungano wa vyama vikuu iliyoingia madarakani mwaka mmoja uliopita mjini Berlin.Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wana maoni tofauti kuhusika na suala kama kipindi hicho cha mwaka mmoja kimeleta tija au la.

Gazeti la NORDKURIER la mjini NEUBRANDENBURG linasifu werevu wa Angela Merkel.Gazeti linaandika:

„Nani aliyefikiria katika mwaka 1990,pale „msichana wa zamani wa Helmut Kohl“,alipojibwaga kwa mara ya kwanza katika jukwaa la kisiasa Ujerumani nzima?Hasa wapinzani wake wa kisiasa,ambao kitu kidogo tuu kikitokea walikua wakimcheka,sasa kijiba kimewasakama-mamoja ni wafuasi wa chama gani cha kisiasa.“

Gazeti la NÜRNBERGER NACHRICHTEN linahisi Angela Merkel angebidi aonyeshe ukakamavu zaidi hasa katika siasa ya ndani au mageuzi ya mfumo wa afya.