1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YEREVAN: Uchaguzi wa Armenia wasifiwa.

13 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2U

YEREVAN

Jopo la wachunguzi wa uchaguzi la Shirika la Ushirikiano na Usalama la Ulaya limesema uchaguzi wa jana wa bunge umeendeshwa vizuri kiasi kuliko chaguzi za awali katika Jamhuri ya Armenia.

Mwanachama mmoja wa jopo hilo amewaambia waandishi wa habari kwamba uchaguzi huo kwa kiasi kikubwa umeendeshwa kufuatana na viwango vya kimataifa.

Maitaifa ya magharibi yalikuwa yameitaka Armenia kuzuia udanganyifu au kutishiwa wapiga kura wakati wa uchaguzi huo.

Wakati huo huo, imebainika chama tawala cha Republican na vyama vyote vinavyomuunga mkono rais wa nchi hiyo yamkini vitashinda uchaguzi huo.

Tume ya uchaguzi imesema miongoni mwa kura asilimia sitini zilizohesabiwa, chama cha Republican kimejishindia zaidi ya asilimia thelathini na tatu wakati ambapo chama kikuu cha upinzani kimepata asilimia 6.