1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZAGREB.Afisa wa cheo cha juu atuhumiwa kwa uhalifu wa kivita

24 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzq

Mahakama nchini Croatia imetoa amri ya kukamatwa mbunge mmoja anaetuhumiwa kwa mauaji ya halaiki ya raia wa Serbia wakati wa uhuru wa Croatia katika miaka ya tisini.

Shirika la habari la taifa la Croatia, Hina limetangaza kuwa mahakama mjini Zagreb imetoa waranti ya kumkamata Branimir Glavas kwa tuhuma za uhalifu wa kivita dhidi ya wa-Serb wakati alipokuwa mkuu wa maswala ya ulinzi mashariki mwa mji wa Osijek.

Glavas ambae amekanusha kuyatenda hayo ni afisa wa cheo cha juu nchini Croatia kuwahi kutuhumiwa kwa uhalifu wa kivita.