1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

3,700 wafa maji waklienda ulaya Mediterania

25 Oktoba 2016

Mashirika ya kutoa misaada yamesema iwakimbizi waliokufa maji katika bahari ya Meditarania karibu kufikia idadi jumla ya waliokufa mwaka jana. Zaidi ya wakimbi 3,700 wamezama katika azma yao ya kufika barani Ulaya.

https://p.dw.com/p/2RgW9
Libyen - Flüchtlinge auf überladenem Boot warten auf Rettung
Wakimbizi wa Libya katika safari hatarishi ya kuvuka Bahari ya Mediterania Picha: Getty Images/AFP/A. Messinis

Wafanyabiashara wa kusafirisha watu kwa njia zisizo halali wanawasafirisha maelfu ya watu kwa vyombo dhaifu vya majini kutoka Libya hadi Italia kwa makundi makubwa kama mojawapo ya njia za kupunguza hatari za kukamatwa lakini pia kama njia ya kufanya vigumu kazi za makundi ya uokozi.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwashughulikia wakimbizi UNHCR limesema kufikia sasa zaidi ya watu 3,740 wamekufa maji ikiwa karibu idadi jumla ya watu 3,771 ya waliokufa mwaka jana wakati zaidi ya wahamiaji na wakimbizi milioni moja walipoamua kufanya safari hatari ya majini kujaribu kuingia katika nchi za Ulaya.

Msemaji wa UNHCR William Spindler amewaambia wanahabari mjini Geneva kuwa idadi ya waathiriwa mwaka huu ndiyo mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika bahari ya Mediterania kwani idadi ya vifo imeongezeka mara tatu ya hali ilivyokuwa katika miaka iliyopita.

Watu zaidi ya 2000 waliokolewa 2015

Mittelmeer Mehr als 6000 Bootsflüchtlinge gerettet
Wakimbizi kutoka katika baadhi ya mataifa ya AfrikaPicha: picture alliance/Pacific Press/A. Di Vincenzo

Askari wa majini wa Italia wamesema takriban wahamiaji 2,200 waliokolewa hapo jana katika shughuli 21 za uokozi na miili 16 iliopolewa. Miili mingine 17 iliopolewa mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwemo ya watoto wanne.

Shirika la kimatifa kuhusu uhamiaji IOM limesema wamepokea taarifa kutoka kwa walioshuhhudia mikasa hiyo kuwa huenda kuna waathirwa zaidi.

Tangu Umoja wa Ulaya na Uturuki kufikia makubaliano mwezi machi mwaka huu ya kufunga njia zinazotumika na wahamiaji nchini Ugiriki, njia ya Libya hadi Italia imekuwa ndiyo inayotumika zaidi na wahamiaji sasa kuvuka bahari ya Meditania na kuingia nchi za Ulaya.

UNHCR inakadiria kuwa kati ya wahamiaji au wakimbizi 47 wanaojaribu kufanya safari ya kuvuka bahari ya Meditarania kati ya Libya na Italia, mmoja hufa maji. Zaidi ya watu laki tatu wamevuka bahari hiyo mwaka huu.

Spindler amesema biashara haramu ya kuwasafirisha watu imekuwa biashara kubwa na inafanywa sasa katika kiwango cha kama cha uzalishaji bidhaa viwandani na sasa wafanyabiashara hao wanatuma boti kadhaa zilizojaa watu kwa wakati mmoja na hivyo kufanya shughuli za uokozi kuwa ngumu kwani wanahitaji kuwaokoa maelfu ya watu walioko katika boti karibu mia.

Wengi wanaofanya safari hiyo inayohatarisha maisha yao ni raia wa Syria, Afghanistan na Iraq wanaokimbia vita nchini mwao na vile vile raia wa kutoka pia nchi za Afrika zinazokumbwa na mizozo na hali mbaya ya kiuchumi.

Mwandishi: Caro Robi/Reuters
Mhariri: Mohammed Khelef