1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watoto millioni 218 wanaendelea kutumishwa duniani

12 Juni 2008

-

https://p.dw.com/p/EIFs
Msichana mdogo akibebeshwa mawe ya ujenzi nchini IndiaPicha: AP

Licha ya kupingwa kufanyishwa kazi watoto duniani bado watoto kiasi millioni 218 wanaendelea kufanyishwa kazi kila siku tena kwa muda mrefu. Watoto wanafanyishwa kazi chini ya mazingira hatari na magumu na baadae wanapata matatizo ya kiafya .Kwa mfano watoto wanatumiwa katika kazi za kufuma mikeka, kuvunja mawe pamoja na ujenzi. Mwaka 1989 Umoja wa mataifa ulipitisha mkataba wa shirika la kimataifa la kazi duniani ILO kupinga kufanyishwa kazi watoto.

Mtu aliyesoma riwaya ya charles Dickens anajua kwamba fikra ya kuwatumia watoto kama nguvu kazi sio geni lakini barani ulaya jambo hilo limeanza kufifia kwani mkataba wa umoja wa mataifa wa mwaka 1989 unapinga kutumiwa watoto kama nyenzo ya kiuchumi.

Lakini katika nchi nyingi za dunia kuna ile fikra kwamba utoto ni hatua ya maisha ambapo mtu anahitaji ajiendeleze kimwili na kiakilikwa hivyo maendeleo yalifikiiwa na jamii ya kimataifa miaka 20 iliyopita ilikubaliana na tafrisri hasa ya neno mtoto kama anavyoelezea Joanne Dunn wa shirika la kimataifa la kuwasaidia watoto UNICEF:

''Watoto ni wale watu walio chini ya miaka 18 kwa mujibu wa mkataba juu ya haki za mtoto.Ufanyishaji kazi watoto unatafsiriwa kama shughuli inayomyima mtoto elimu na ina madhara makubwa katika maendeleo.''

Kuanzia umri wa miaka 14 mtoto huyo hapaswi kutumiwa kufanya kazi kwa lengo la kuleta faida na kuanzia mtoto wa miaka 15 anaweza kufanyishwa kazi tu katika sekta zisizokuwa za hatari.Lakini pamoja na kufikiwa mkataba wa shirika la kimataifa la kazi duniani ILO takriban watoto millioni 218 wanaendelea kufanyishwa kazi kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi zao.Watoto hao wengi wanatumiwa kafanya kazi mbaya kama anavyosema Frank Hagemann kutoka shirika la ILO ambalo linapigania kuondosha kabisa utumiaji watoto makazini.

''Kwanza inahusu watoto kufanyishwa za ukahaba,ujakazi majumbani,wanatumiwa vitani pia wanalazimishwa kufanya kazi za sulubu na hiyo naamini ndo kazi kubwa wanayoshirikishwa watoto ambayo ni ya hatari.Zaidi ya asilimia 90 ya watoto wanafanyishwa kazi hizo za hatari.''

Umaskini ndio chanzo kikubwa cha tatizo hilo na ndo sababu watoto duniani wanalazimika kufanya kazi.Makampuni mengi na biashara nyingi zinapendelea kuaajiri watoto kwasababu wanakubali kima cha chini cha mishahara na maridhia kuliko watu wazima na pia hawajiandikishi katika vyama vya kutetea maslahi ya wafanyikazi. Wazazi wengi wanapendelea kuwapeleka shule watoto wao kuliko kuwaachia wafanye kazi ikiwa wanauwezo.Lakini mara nyingi wazazi hao hawana budi anasema Frank Hagemann kutoka shirika la ILO na hapa akitoa mfano anasema.

" Hilo ni tatizo kubwa barani Afrikasio tu kwa wasichana lakini pia kwa wavulana kutokana na janga la maradhi ya ukimwi na virusi vya HIV,.Na wazazi wanajitahidi wasife haraka kwahivyo mara nyingi wanakuwa wagonjwa na kukosa nguvu za kufanya kazi.Kwa hivyo watoto hao wanakuwa hawawezi kuwasaidia wazee wao katika kazi za nyumba ila wanabidi kufanya kazi za kutafuta riziki.Hiyo bila shaka ni kuwafanyisha kazi watoto.''

Nchini Msumbiji katika maeneo kunakolimwa tumbaku idadi ya watoto wanaoacha masomo ni kubwa mno kuliko maeneo mengine nchini humo.Hii ni kwasababu wengi wanakimbilia kufanya kazi katika mashamba ya tumbaku ili wajipatie fedha na hii inaonyesha wazi kwamba ufanyishaji kazi watoto unachangia sana katika kudidimiza elimu kwa watoto nchini humo.