1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zanzibar: Hali ya viongozi wa Uamsho gerezani

8 Novemba 2012

Viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar wanakabiliwa na hali mbaya gerezani.

https://p.dw.com/p/16fLS
Baadhi ya viongozi wa Uamsho waliotiwa gerezani
Baadhi ya viongozi wa Uamsho waliotiwa gerezaniPicha: DW

Mawakili wa Viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI ) wamesema hii leo kuwa wateja wao waliokamatwa siku 17 zilizopita kwa tuhuma za kuchochea vurugu kisiwani Unguja, hawatendewi haki na wanapata mateso makubwa gerezani wanakoshikiliwa.

Mawakili hao wakiongozwa na Salim Tawfiq wanasema kwa sasa wateja wao hawapaswi kutendewa visa kama hivyo kwa kuwa bado ni watuhumiwa na kwamba hawajatiwa hatiani.

Muda mfupi uliopita Amina Abubakar amezungumza na wakili Salim Tawfiq na kwanza anaelezea zaidi juu ya mateso hayo wanayopata wateja wake.

(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi Amina Abubakar

Mhariri Yusuf Saumu