1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zanzibar kubadili katiba kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa

Josephat Nyiro Charo2 Agosti 2010

Baraza la wawakilishi Zanzibar linatarajiwa kukutana kuibadili katiba baada ya kura ya maoni kuunga mkono serikali ya umoja wa kitaifa visiwani humo baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 31 mwaka huu

https://p.dw.com/p/Oa5H
Rais wa Zanzibar, Aman Abeid KarumePicha: AP Photo

Katika kura ya maoni iliyofaywa Visiwani Zanzibar, huko Tanzania, mwishoni mwa wiki kuwauliza wananchi kama wanataka katiba ya nchi yao ibadilishwe ili kuweko serekali ya Umoja wa taifa baada ya uchaguzi mkuu ujao mwezi Oktoba mwaka huu, asilimia 66.4 ya wapiga kura walisema wanaunga mkono jambo hilo, na waliobakia walisema hawataki.

Hiyo ina maana Baraza la Wawakilishi visiwani humo litakutana kuibadilisha katiba ya Zanzibar ili kuweka njia wazi ya kuweko serikali ya Umoja wa taifa, huenda sana baina ya vyama vya CCM na CUF.

Othman Miraji alizungumza na mkuu wa upinzani katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hamad Rashid Mohammed, ambaye yumo katika uongozi wa Chama cha CUF.

Pia alizungumza na Harun Suleiman, waziri wa elimu wa Zanzibar, na mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama tawala cha CCM.