1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya Baba mtakatifu Afrika na Ukimwi

18 Machi 2009

Ni mada iliochambuliwa na wahariri leo:

https://p.dw.com/p/HEit
Pope Benedict XVIPicha: AP

Maoni ya wahariri wa magayzeti ya Ujerumani hii leo yametuwama zaidi katika mada za ndani ya nchi.Moja hata hivyo inazungumzia ziara ya baba Mtakatifu ilioanza jana barani Afrika.Mada nyengine ya nje ya nchi ni ziara ya Marekani ya waziri wa uchumi Zu Guttenmberg katika juhudi zake za kuliokoa kampuni la magari la OPEL kutoka kampuni mama la General Motors.

Gazeti la EMDER ZEITUNG laandika:

"Matamshi ya hivi punde aliotoa Baba mtakatifu katika ziara yake hii ya Afrika kuwa matumizi ya kondom yanazidisha kueneza maradhi ya UKIMWI,yanastusha na hayafahamiki........Mayatima milioni 3.6 walioachwa na wazee wao waliofariki kwa UKIMWI kwa mfano, waliopo barani Afrika,kutouona huko ukweli wa hali ya mambo hakuwasaidii kitu.Hawahahitaji nasaha za nadharia ya kanisa , bali msaada halisi."Likiendeleza zaidi visa vya kutatanisha vya baba mtaklatifu,gazeti la NEUE ZEITUNG linakumbusha:

"Kwanza ilikua kisa cha ( kasisi) Williamson na sasa hiki cha UKIMWI: Msimamo anaouchukua Baba mtakatifu Benedikt sio tu unamtenga na msingi wake mwenywe anaosimamia- waumini, bali pia zaidi na viongozi wengine kanisani........

Hakuna mwanasiasa anaezungumza na Baba mtakatifu kwa kuhofia akifanya hivyo, huenda asichaguliwe."

Likitukamilishia mada hii, gazeti la Kolnerstadt-Anzeiger laandika kwamba, wakati mashirika ya Umoja wa Mataifa na ya kibinafsi yanapigia upatu matumizi rahisi kabisa na madhubuti ya kujikinga na UKIMWI kwa kutumia vipira (Kondom) na kuzuwia kushika mimba isiotakiwa, Baba mtakatifu anafunga safari kutoka Roma na kuhubiri kinyume chake.

Gazeti la Nuremberger Zeitung latuchukua katika hatima ya kiwanda cha magari cha OPEL kinachopepesuka.Laandika:

Kwa safari alofunga waziri wa uchumi wa Ujerumani Karl-Theodor zu Guttenmberg, nchini Marekani kuliokoa kampnu la magari la OPEL kutoka makucha ya kampuni mama la GM ,matokeo ya mazungumzo yake huko si makubwa hivyo.Badala ya kujitoa wazi mshindi kufuatia mazungumzo yake na vigogo vya GM,amejitokeza na ahadi za mdomo tu . Hatahivyo, laona gazeti, Ujerumani imejipatia tena waziri wa uchumi anaietamba na wa kujitembeza.Pekee sifa hizo ni maendeleo.

Ama gazeti la Westdeutsche Zeitung kutoka Dusseldorf laandika:

"Kusema kweli, risala ya waziri zu Guttenmberg ,Marekani imefika ilikokusudiwa na si kasoro wala zaidi.Ujerumani imepania kutoburuzwa na Washuington .Kwa wananchi wa Ujerumani ,kujiamini huko kumepokewa uzuri.Mameneja wa GM huko Detroit,hadi sasa hawakutoa matumaini ya kutegemeka ya mustakbala mwema wa kiwanda hiki cha magari.Na hii inazusha hofu na kukatisha tamaa upande huu wa pili wa bahari ya Atlantik ."

Muandishi Ramadhan ali

Mhariri: O.Miraji