1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya Gaddafi Paris

12 Desemba 2007

Ziara ya Kiongozi wa Libya nchini Ufaransa na haki za binadamu.

https://p.dw.com/p/CaiR
Nicolas Sarkozy na A.MerkelPicha: AP

Kitambo kirefu sasa hakuna ziara iliozusha vumbi kubwa nchini Ufaransa kama hii ya siku 5 ya Kiongozi wa Libya Muamar Gaddafi.Kwamba licha ya ila kali hata kutoka kwa wenzake, rais Nicolas Sarkozy,amempokea Gaddafi mjini Paris,yabainisha jinsi alivyovinjari kutekeleza sera zake za kujenga ushirikiano wa nchi zinazopakana na Bahari ya kati (Medditerranian).

Ushirikiano huo anaolenga Sarkozy, ni wa kiuchumi ukiingiza pia sekta ya nguvu za atomiki.

Uchambuzi wa Peter Philipp,mhariri wetu wa maswali ya

Swali la haki za binadamu litakua nguzo ya sera zake kama rais wa Ufaransa-aliahidi Sarkozy kileleni mwa kampeni ya uchaguzi uliom leta madarakani nchini Ufaransa.Nusu mwaka baada ya kuchaguliwa baadhi ya mawaziri wake wanamtuhumu kwamba Sarkozy, amesahau ahadi hizo alizotoa.

Chanzo cha ila hizo ni ziara ya sasa nchini Ufaransa ya Kiongozi wa Libya Muamar Gadhafi ambae alipokewa rasmi mikono 2 na rais sakozy hata ile siku yenyewe ya kuadhimisha haki za binadamu.Sarkozy, haoneshi kukereka na ila kama hizo kwani kichwani mwake ana ajenda nyengine: Kujipatia mikataba minono ya mabilioni kadhaa kutoka Libya –kuanzia kinu cha kugeuza maji ya chumvi kuwa maji ya kunywa hadi kuiuzia Libya madege chapa Airbus na hata silaha na vinu vya atomiki.

Kama wanasiasa wengine wanaojikuta katika hali kama hii,Sarkozy anasisitiza kwamba amelizusha pia swali hilo la kukanyagwa haki za binadamu nchini Libya katika mazungumzo yake na Gaddafi.

Rais wa Libya lakini amekanusha kwamba swali la haki za binadamu halikuwa kamwe mada ya mazungumzo yao.

Hakuna lakini sababu ya kufurahia hali hii katika miji mingine ya Umoja wa Ulaya ingawa huko tangu kushika madaraka ya urais kwa sarkozy,wasi wasi umeingia juu ya mkondo wa siasa zake. Sarkozy anagutuka tu kuchukua hatua na kwamba eti hashauriani na wenzake kwanza kabla kuchukua hatua.Anatanguliza masilahi yake binafsi na ya nchi yake Ufaransa na anajitenga mbali sana na wenzake katika baadhi ya maswali walioafikiana.

Ila dhidi ya Sarkozy katika nchi zanachama wa UU ni za kadiri fulani tu na si kubwa hivyo.Pia na hasa nchini humu Ujerumani.Ufaransa ikiuza ndege za airbus au silaha ,hunufaika pia viwanda na makampuni ya Ujerumani na hata kero zilozushawa na hatua za Sarkozy.

Endapo mikakati inayofuatwa ni ya kero za kisiasa tu na haina manufaa ya kiuchumi au biashara,basi ila huwa kali.Ndio mana zinasikika ila hizo katika mradi wake wa ushirikiano wa nchi za bahari ya Mediterranian .Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani , anahisi mkakati wa Qasri la Elysee kuelekea nchi za bahari ya kati kimsingi waweza ukabomoa msingi unaosimamia Umoja wa Ulaya.Sarkozy analenga shabaha gani katika mkatati huo ?

Ni kujenga usuhuba mwema na nchi za Afrika ya kaskazini n a hasa zile zinazotoa mafuta mfano wa Libya na Algeria wakati huo huo kuzuwia kujiunga na Umoja wa Ulaya kwa n chi ya bahari ya kati Uturuki .Mahala pake ni kuunda Umoja wa nchi za bahari ya kati kuzivutia nchi za Afrika ya kati kuungamkono mkakati wake kila turufu atayoitumia ni halali.

Kwahivyo chini ya mkakatio huo katika swali la nishati ya atomiki kuhusu Iran,Sakorzy amejitupa upandewa Marekamni .Katika Afrika ya kaskazini na Mashariki ya kati ,Sarkozy yutayari kuzipa ufundi wa nishati ya kinuklia nchi kama Misri, Libya,Tunesia,Algeria na hata Morocco.

Kwamba Iran inatapia kumiliki silaha za atomiki hakuna awezae kutoa ushahidi ,lakini tuhuma tu za aina hiyo zimetosha kwa baadhi ya nchi katika ghuba na mashariki ya kati kupanga nazo miradi kama hiyo.

Kwa rais Sarkozy, hii yalingana na mkakati wake.

Rais sarkozy wa Ufaransa kama wanaomkosa wanavyo kejeli: atatimiza shabaha yake ya ushirikiano na nchi za bahari ya kati pale nchi za kiislam u zwa mwabao huo zimepatiwa vinu vya atomiki kutoka Ufaransa.