1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya kiongozi wa Hamas anaeishi uhamishoni,Khaled Meshaal

Oumilkher Hamidou7 Desemba 2012

Kiongozi wa Hamas anaeishi uhamishoni Khaled Meshaal anautia mguu katika ardhi ya Palestina huko Gaza, kwa mara ya kwanza baada ya miaka 45, kushiriki katika "Mkutano wa ushindi" dhidi ya Israel.

https://p.dw.com/p/16xTe
Ismael Hanniyeh apeana mkono na Khaled Meshaal(kulia)Picha: Reuters

Khaled Meshaal anatarajiwa kuwasili Gaza wakati wowote kutoka sasa, kupitia kituo cha mpakani cha Rafah kinachoiunganisha Gaza na Misri. Atapokelewa na Ismael Hanniyeh anaeiongoza serikali ya Hamas tangu kundi hilo la itikadi kali liliponyakuwa madaraka katika eneoi hilo mwaka 2006.

Baadae viongozi hao wawili wanatarajiwa kushiriki kwa pamoja katika mkutano na waandishi habari kabla ya kuitembelea nyumba ya muasisi wa Hamas, Sheikh Ahmed Yassin aliyeuliwa na Israel mwaka 2004.

Mamia ya polisi na vikosi vya usalama na wanamgambo wa tawi la kijeshi la Hamas,Ezzedine Al Qassam wamewekwa katika njia ya Salahedine inayouunganisha ukanda wa Gaza kutoka kaskazini hadi kusini-njia atakayopitia kiongozi huyo wa Hamas anaeishi uhamishoni pamoja na wenzake.

Mkuu wa chama cha Jihad,Ramadhan Challah ambae pia alitaka kuja Gaza kushiriki katika mkutano huo wa ushindi"ameakhirisha safari yake baada ya kutolewa onyo na Israel dhidi yake.

Israel Palästina Gaza Konflikt Waffenruhe
Wapalastina washerehekea makubaliano ya kuweka chini silahaPicha: AP

Khalked Michaal amepangiwa kusalia kwa saa zisizozidi 48 huko Gaza na kushiriki kesho katika "Mkutano mkubwa kabisa,"kusherehekea ushindi,na kuadhimisha miaka 25 tangu vugu vugu la Intifadha lilipoanza na wakati huo huo tangu Hamas ilipoundwa.

Kiongozi huyo wa Hamas,Khaled Michaal ambae hajawahi kuikanyaga ardhi ya wapalastina tangu alipolihama eneo la ukingo wa magharibi la Mto Jordan,akiwa na umri wa miaka 11,amepata nguvu kisiasa baada ya mapigano ya siku nane katika eneo hilo linalozingirwa.

Ziara ya Khaled Mechaal ambae cheo chake kinabishwa na baadhi ya viongozi wa Hamas huko Gaza, inatokea katika wakati ambapo matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa ndani wa chama hicho ulioanza tangu miezi kadhaa iliyopita,bado hayajulikani.Yeye mwenyewe mara kadhaa amekuwa akielezea azma ya kuachana na madaraka aliyo nayo.

Tellawi)
Khaled MeschaalPicha: AP

Kiongozi huyo mwenye haiba aliyechangia katika kufikiwa makubaliano ya kuweka chini silaha kati ya Israel na Hamas mwezi uliopita nchini Misri,anaonyesha kuregeza msimamo wake kuelekea suala la amani ya mashariki ya kati.Anaunga mkono pia juhudi za kuwapatanisha wapalastina wenyewe kwa wenyewe. .

Hata wadadisi wa Israel wanazitaja juhudi zake kuwa ni za kutia moyo katika utaratibu wa kusaka amani .

Mwandishi: Hamidou Oummilkheir/Reuters/AFP

Mhariri: Mohammed Khelef