1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zuma aendelea kugonga mwamba

Sekione Kitojo
19 Juni 2017

Idara ya kupambana na rushwa nchini Afrika kusini  itapinga juhudi za rais wa nchi hiyo Jacob Zuma kutaka ripoti ya madai ya kuwapo  ushawishi kwake binafsi na serikali yake iwekwe kando.

https://p.dw.com/p/2exhd
Joyce Busisiwe Mkhwebane Public Protector Official Photo
Picha: GCIS

Mwendesha  mashitaka  mkuu  wa  serikali  Busisiwe Mkhwebane  amesema  leo, kwamba  idara  ya kupambana  na  rushwa  nchini  Afrika  kusini  itapinga juhudi  za  rais  wa  nchi  hiyo  Jacob Zuma kutaka  ripoti ya  madai  ya  kuwapo  ushawishi  kwake  binafsi  na serikali  yake  iwekwe  kando.

Thuli Madonsela, mrithi  wa Mkhwebane  katika  wadhifa wa  mwendesha  mashitaka  aliitoa  ripoti  hiyo  mwezi Novemba. Ilitaka  ufanyike  uchunguzi  wa  mahakama kuhusiana  na  madai  kuwa  Zuma , baadhi  ya  mawaziri na  baadhi  ya  makampuni  ya  taifa  yalichukua  hatua kinyume  na  utaratibu , lakini  ripoti  hiyo  haikwenda umbali wa  kueleza  kwamba  uhalifu ulitendeka.

Mwezi  Desemba  mwaka  jana  Zuma, ambaye  amekama kutenda  kosa  na  kukataa  miito  wa  kutaka  ajiuzulu kuhusiana  na  kashfa  kadhaa  ambazo zimeikumba serikali  yake, aliitaka  mahakama  kuu  kuweka  kando ripoti hiyo.