Deutsche Welle: Kwa uchache watu wanane wahofiwa kufariki dunia na wengi zaidi hawajuilikani walipo kufuatia ajali ya boti kwenye kisiwa cha Lamu nchini Kenya.
Zaidi ya asilimia 90 ya shule nchini Kenya zimefunguliwa leo, baada ya kufungwa kwa takribani wiki mbili kutokana na mafuriko yaliyosababisha vifo vya watu 270.
Kundi moja la mataifa ya Afrika limetoa wito wa kuwepo kwa mkataba wa kimataifa kuhusu kulinda raslimali za vinasaba na elimu ya kiasili, utakaoweka vikwazo kwa kampuni zitakazoukiuka mkataba huo.
Mvua kubwa zilizoambatana na mafuriko zimeacha athari za kiafya kwa watoto wengi katika maeneo ya mabanda nchini Kenya