Deutsche Welle: Madaktari wa hospitali za umma nchini Kenya wamaliza mgomo wao baada ya serikali kukubaliana nao juu ya kutekeleza matakwa ya madaktari hao.
Watu wasiopungua 188 wamekufa nchini Kenya kufuatia mafuriko na maporomoko ya ardhi tangu mwezi Machi, huku wengine karibu 200,000 wakilazimika kuyahama makazi yao.
Rais wa Kenya William Ruto ameahirisha mpango wa kuzifungua tena shule wiki ijayo hadi kutakapotolewa tangazo jingine, wakati mvua kubwa na mafuriko yaliyowaua watu zaidi ya 200 yakiendelea.
Sehemu kubwa ya Tanzania ilikosa umeme siku ya Jumamosi wakati mvua kubwa na pepo kali za Kimbunga Hidaya kikikaribia kuipiga nchi hiyo ya Afrika Mashariki kufuatia wiki kadhaa za mafuriko kwenye ukanda huo.