Deutsche Welle: Katika mechi za kugombania nafasi ya kuingia Ligi Kuu ya Ulaya hapo kesho, Zurich itaumana na Vaslui, Lazio na Sporting Lisbon na Besiktas na Stoke City
Mabingwa wa Ligi ya Ulaya Europa League Eintracht Frankfurt wanakaribia kumsajili kiungo wa zamani wa Borussia Dortmund na Bayern Munich Mario Götze kutoka PSV Eindhoven ya Uholanzi.
Timu inayoshiriki Ligi Kuu ya kandanda ya Ujerumani, Bundesliga ya Eintracht Frankfurt ndio mabingwa wa mwaka huu, wa kombe la ligi ya Ulaya, Europa League, baada ya kuifunga timu ya Rangers kutoka Scotland kwa mabao matano kwa manne kupitia mikwaju ya penalti. Grace Kabogo amezungumza na mwandishi wa zamani wa DW na mchambuzi wa kandanda, Sekione Kitojo. kwanza anaeleza
Droo ya 16 bora ya ligi ya mabingwa imeshuhudia timu nane zilizomaliza katika nafasi ya juu kwenye makundi zikipangwa dhidi ya mmoja wa washindi nane waliomaliza nafasi ya pili.