Deutsche-Welle:Uingereza itaitisha warsha kuhusu haki za binaadam nchini Libya,kuisaidia serikali ya mpito ikabiliane na vituko vya makundi ya waasi nchini humo.
Shirika la Uhamiaji Duniani IOM limetoa ripoti ya utafiti uliobanisha kuwa zaidi ya watu 63,000 wamepotea ama kutoweka kwa uhamiaji duniani kwa kipindi cha muongo mmoja huku vifo vingi vikitokana na kuzama majini
Juhudi za kimataifa zimeshika kasi kuisadia Libya kufuatia janga baya kabisa la mafuriko yaliyosababisha vifo vya watu karibu 4,000 na kuwaacha wengine maalfu wakiwa hawajulikani waliko. Vifo huenda vikafikia 20,000.
Mapigano kati ya makundi hasimu ya wanamgambo kwenye mji mkuu wa Libya, Tripoli, yamewauwa watu 27 na kuwajeruhi zaidi ya 100, yakitajwa kuwa mapigano makubwa kabisa tangu mwaka huu uanze.