Deutsche Welle: Kikosi cha kwanza cha wanajeshi 100 kutoka Djibouti kimewasili Mogadishu jana kuungana na vikosi vya Umoja wa Afrika nchini Somalia, AMISOM.
Utawala wa kijeshi wa Burkina Faso umevipiga marufuku vyombo vya habari zaidi vya kimataifa, ikiwa ni pamoja na DW. Hatua hii ni sehemu ya mtindo wa ukandamizaji wa vyombo vya habari.
Waandishi wa habari Tunisia pamoja na viongozi wa upinzani wameelezea wasiwasi wao juu ya kuongezeka kwa mashitaka dhidi yao tangu Rais Kais Saed alipotoa amri ya kuharamisha "habari za uongo."
Ukraine yaishukuru Vatican kwa juhudi za kujaribu kuwarudisha maelfu ya watoto waliopelekwa Urusi, ujumbe wa MONUSCO wasitisha operesheni zake jimboni Kivu Kusini katika jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Uingereza yawawekea vikwazo wanasiasa wa Uganda kutokana na madai ya ufisadi