Deutsche Welle: Watu wanaoushukiwa kuwa wafuasi wa kiongozi wa zamani wa Libya, Marehemu Muammar Gaddafi, wameuvamia mji wa Bani Walid na kuua watu saba.
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa mripuko wa magonjwa kaskazini mashariki mwa Libya, ambako maelfu ya watu wamekufa kutokana na mafuriko, unaweza kusababisha mzozo wa pili mbaya zaidi kwa taifa lililosambaratika kwa vita.
Idadi iliyokadiriwa ya vifo katika mji wa Derna nchini Libya baada ya mafuriko makubwa huenda ikaongezeka maradufu na kufikia 18,000 hadi 20,000. Hayo ni kulingana na Meya wa mji wa Derna, Abdulmenam Al-Ghaithi.
Mkuu wa shirika la kimataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya nyuklia (IAEA) Rafael Grossi amesema takriban tani 2.5 za madini ya urani zimetoweka bila maelezo kwenye kituo kimoja nchini Libya.