1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

8 viongozi wa kikoo wauawa Pakistan

7 Januari 2008
https://p.dw.com/p/ClN6

ISLAMABAD:

Watu wanaoshukiwa kuwa waislamu wa msimamo mkali wamewauwa kwa kupiga risasi viongozi wa kiukoo wanane ambao wamejihushisha katika juhudi za kujaribu kusitisha mapigano kati ya vikosi vya usalama na wapiganaji wa chini kwa chini katika maeneo ya kaskazini magharibi mwa Pakistan.

Maafisa wanasema kuwa watu hao waliuliwa katika matukio tofauti jumapili na mapema jumatatu katika Waziristan kusini,eneo lenye milima lililo karibu na mpaka wa Afghanistan ambako wapiganaji wa Kitaliban na Al-Qaida wannaminika kujificha.

Jeshi linasema kuwa washukiwa wakiislamu waliwauwa watu watatu katika ofisi moja ilioko Wana, mji mkuu wa jimbo hilo.

Wengine watano waliuliwa katika matukio tofauti.Watu hao waliouliwa walikuwa wakutane jumatatu kujadili majadilano ya amani kati ya vikosi vya serikali ya Pakistan na wapiganaji.