1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABIDJAN:Wanajeshi wa kulinda usalama waliohusika na unyanyasaji wa kijinsia kuadhibiwa

24 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfp

Umoja wa mataifa unatangaza kuwa mwanajeshi yoyote wa kulinda amani kutoka nchi ya Morocco ,atakayepatikana na hatia ya kuhusika na unyanyasaji wa kijinsia nchini Ivory Coast atarejeshwa kwao na kuadhibiwa kulingana sheria za nchi yake.Kikosi cha majeshi 730 kiliagizwa kubakia katika kambi yake ya mjini Bouake muda mfupi baada ya Umoja wa mataifa kupokea taarifa za madai ya kuwanyanyasa watoto kijinsia.

Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa mataifa Margherita Amodeo.Msemaji huyo anaongeza kuwa ni kitengo kimoja pekee cha kikosi hicho ndicho kilichohusika na madai hayo.Umoja wa mataifa ulitoa taarifa rasmi Ijumaa iliyopita katika makao yake makuu mjini Newyork,Marekani.Uchunguzi wa Shirika hilo ulibaini kuwa madai hayo yalikuwa ya kweli na kuamua kusimamisha shughuli za kikosi hicho.