1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ajiripua kwa kubamiza gari dhidi ya basi la shule

10 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZiV

ISLAMABAD

Mshambuliaji wa kujitolea muhanga maisha amelibamiza gari lililosheheni mabomu dhidi ya basi la shule karibu na kambi ya kikosi cha anga kaskazini magharibi mwa Pakistan leo hii na kujiuwa yeye mwenyewe na kujeruhi watu tisa wakiwemo watoto watano.

Msemaji wa kijeshi Meja Generali Waheed Arshad amesema gaidi amelishambulia basi la shule ambapo dereva na mlinzi aliekuwa amekaa mbele wamejeruhiwa vibaya sana.

Shambulio hilo linakuja siku moja baada mshambuliaji wa kujitolea muhanga maisha kulibamiza gari lilosheheni mabomu kwenye kituo cha ukaguzi wa polisi katika bonde la Swat kaskazini magharibi mwa nchi hiyo na kuuwa watu sita.