1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ALGIERS:Jeshi lauwa wapiganaji wa Kiislamu

15 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC20

Jeshi la Algeria lililoshika doria limewauwa wapiganaji wawili wa Kiislamu katika operesheni iliyofanywa mashariki mwa mji mkuu ikiwa ni siku tatu kabla ya uchaguzi wa wabunge kufanyika.Kwa mujibu wa maafisa wa serikali mpiganaji wa tatu alijeruhiwa na wanajeshi hao waliokamata na kuzuia bunduki na vifaa vya mawasiliano waliposaka eneo la Boumerdes ulio kilomita takriban 50 kutoka mji mkuu.

Jeshi la Algeria linaripoti kuwaua wapiganaji wengine tisa katika eneo hilohilo aidha eneo la Tizi Ouzou lililo karibu.Ghasia hizo zinatokea ikiwa ni siku tatu kabla uchaguzi kufanyika huku kundi linaloshirikiana na Al Qaeda likitoa wito kwa wapiga kura kuususia.

Kundi la wapiganaji la GSPC lilibadili mtizamo wake mwanzoni mwa mwaka huu kama sehemu ya kundi la magaidi la Al Qaeda.Mwezi jana lilikiri kutekeleza mashambulio ya mabomu mjini Algiers yaliyosababisha vifo vya watu 30.

Kwa mujibu wa vyama vya kisiasa wapiga kura hawatasusia uchaguzi huo ambao hautarajiwi kumwondoa Rais Abdelaziz Bouteflika aliye na umri wa miaka 70 na ushawishi mkubwa.