1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMSTERDAM: Bunge la Uholanzi laomba uchunguzi juu ya mateso yaliofanyiwa wafungwa nchini Irak

18 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCrl

Bunge la Uholanzi limeomba kufanyike uchunguzi juu ya taarifa kwamba wachunguzi wa kijeshi wa upelelezi wa Uholanzi waliwatesa wafungwa wa kiiraki mwaka wa 2003. Taarifa hizo zimechapishwa katika gazeti litolewalo kila siku la Volksrant, ikiwa ni siku 5 tu kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini humo. Wachunguzi hao wa kijeshi wa Uholanzi wanasemekana waliwatesa wafungwa wa kiiraki kwa kuwafunika nyuso, kuwamwagia maji ili wasilie macho na kuwasumbua na kelele wakati wa mahojiano.

Waziri mkuu kutoka chama cha Christian Democrate, Jan Peter Balkenende, aliunga mkono uvamizi wa Marekani dhidi ya Irak mwaka 2003 na kuwatuma wanajeshi, lakini aliwarejesha nyumbani miaka miwili baadae wakati yakipamba moto machafuko ya kikabila.

Inaarifiwa kuwa mateso hayo yalitendeka mnamo mwezi Novemba mwaka 2003 katika mkoa wa Al Muthanna kaskazini mwa Irak ambako wanajeshi 1,300 kutoka Uholanzi walikuwa wamepiga kambi.