1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMadagascar

Andry Rajoelina achaguliwa tena kuwa rais wa Madagascar

25 Novemba 2023

Tume ya uchaguzi yasema Rajoelina mwenye umri wa miaka 49, amepata asilimia 58.95 ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi iliyofanyika Novemba 16.

https://p.dw.com/p/4ZRBj
Rajoelina mwenye umri wa miaka 49, amepata asilimia 58.95 ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi iliyofanyika Novemba 16
Rajoelina mwenye umri wa miaka 49, amepata asilimia 58.95 ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi iliyofanyika Novemba 16Picha: Ako Randrianarivelo/IMAGO/ZUMA Wire

Tume ya uchaguzi nchini Madagascar imetangaza hii leo kuwa rais aliyopo madarakani Andry Rajoelina ameshinda kwa mara nyingine katika duru ya kwanza ya uchaguzi ambao ulisusiwa na takriban wagombea wote wa upinzani.      

Tume hiyo imesema Rajoelina mwenye umri wa miaka 49, amepata asilimia 58.95 ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi iliyofanyika Novemba 16.

Idadi ya waliojitokeza kupiga kura ilikuwa ndogo baada ya wagombea 10 kati ya 12 wa upinzani kutoa wito wa kususia uchaguzi huo wakilalamika kuwa ni "mapinduzi ya kitaasisi" kwa faida ya mgombea aliye madarakani.