1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA: Idadi ya vifo kufuatia shambulio la bomu yafikia sita

23 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzC

Idadi ya vifo vilivyosababishwa na mlipuko mkubwa wa bomu katikati mwa mji mkuu wa Uturuki, Ankara, imefikia sita, akiwemo raia mmoja wa Pakistan. Watu wengine takriban 80 wamejeruhiwa katika hujuma hiyo.

Duru za polisi zinasema mlipuko huo, uliovunja vioo vya madirisha ya majengo yaliyo karibu, ulitokea kwenye kituo cha basi wakati abiria wengi walipokuwa wakisubiri usafiri.

Kufikia sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na shambulio hilo. Hata hivyo, waasi wa kikurdi, waasi wa mrengo wa kushoto na waislamu wenye siasa kali, wamewahi kufanya mashambulio ya mabomu nchini Uturuki.