1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA: Mahakama ya katiba yatakiwa ifutilie mbali ombi la upinzani

1 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5e

Mtaalamu wa sheria nchini Uturuki ameishauri mahakama ya katiba nchini humo ikatae ombi la upinzani la kutaka uchaguzi wa rais ufutwe nchini humo. Hayo ni kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Uturuki.

Uamuzi wa mahakama hiyo utaamua hali ya baadaye ya serikali ya waziri mkuu, Reccep Tayyip Erdogan, ya misingi ya dini ya kiislamu inayopingana na Waturuki wasiokumbatia sana dini wakihofia kuna njama ya kuibadili Uturuki kuwa taifa la kiislamu.

Hikmet Tulen, mtaalamu wa sheria aliyepewa kazi ya kuchunguza ombi la upinzani na mahakama ya katiba, ameishauri mahakama hiyo ilitupilie mbali ombi hilo.

Maafisa wa mahakama hiyo hawajatoa matamshi yoyote kuhusiana na ripoti hiyo. Mahakama ya katiba inatarajiwa kutoa uamuzi wake baadaye leo au kesho Jumatano.