1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Makamo wa rais wa zamani kunyongwa

15 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIl

Mahkama ya Rufaa nchini Iraq imeshikilia hukumu iliotolewa na Mahkama Kuu nchini humo ya kumnyonga Taha Yassin Ramadhan makamo wa rais wa zamani wa Saddam Hussein na kwamba adhabu hiyo inaweza kutekelezwa wakati wowote ule.

Ramadhan alikuwa amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani hapo mwezi wa Novemba kwa dima aliyotimiza katika mauaji ya Washia 148 katika mji wa Dujail katika miaka ya 1980 ambayo kwa ajili hiyo Saddam na washauri wake wawili wa zamani walinyongwa.

Lakini mahkama ya rufaa ilipendekeza ahukumiwe kifo na kuirudisha tena kesi hiyo mahkamani.

Kwa mujibu wa sheria ya Iraq hukumu hiyo ya kunyongwa lazima itekelezwe katika kipindi kisichozidi siku 30.