1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mfungwa wa Kiiraki amefariki jela

14 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2z

Mfungwa wa Kiiraki amefariki katika jela inayoongozwa na Marekani kusini mwa Irak. Inasemekana mfungwa huyo labda amefariki kutokana na ugonjwa wa moyo,lakini maiti itafanyiwa uchunguzi kujua sababu halisi ya kifo.Marehemu huyo hakutajwa kwa jina.Kiasi ya wafungwa 13,000 wamezuiliwa katika jela zinazoongozwa na majeshi ya madola shirika nchini Irak.Miongoni mwa wafungwa hao kuna watu wazima waliowahi kuwa na vyeo katika serikali ya zamani ya Saddam Hussein iliyopinduliwa.