1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mmuagiko wa damu unaendelea Irak

26 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXs

Hadi watu 34 wameuawa na wengi wengine wamejeruhiwa katika mfululizo wa miripuko ya bomu iliyotokea katika mji mkuu wa Irak,Baghdad.Katika shambulio moja peke yake,si chini ya watu 20 waliuawa baada ya bomu lililotegwa kwenye gari kuripuliwa kwenye eneo la maduka mengi,kati kati ya mji mkuu Baghdad.Mripuko huo ulitokea muda mfupi baada ya makombora mawili kuvurumishwa kwenye eneo lenye majengo ya serikali na balozi za kigeni ambalo hulindwa vikali.Hapo awali mjini Baghdad,watu 4 waliuawa baada ya pikipiki kurupuliwa sokoni kulikojaa watu.