1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mmuagiko wa damu unaendelea nchini Irak

14 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2r

Si chini ya watu 13 wameuawa katika machafuko mbali mbali nchini Irak.Wakati huo huo polisi wamekuta maiti 7 zilizokatwa vichwa na kutupwa kaskazini mwa mji mkuu Baghdad,ikidhaniwa kuwa hayo ni mauaji ya kulipiza kisasi katika machafuko ya kimadhehebu nchini humo.Katika shambulio jingine,mabomu mawili yaliripuka kati kati ya Baghdad kwenye uwanja wa kuegeza magari. Mtu mmoja aliuawa na wengine 4 walijeruhiwa katika shambulio hilo la bomu.Mripuko huo wa mabomu yaliofichwa ndani ya magari mawili, ulisababisha magari mengine yalioegezwa katika uwanja huo kushika moto pamoja na jengo lililokuwa karibu.Mapema alfajiri,katika mji wa Mahmoudiya,kusini mwa Baghdad,familia ya Kishia ya watu wanne iliuawa baada ya kuvamiwa na washambuliaji waliovaa sare za kijeshi.