1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Rais wa Irak, Jalal Talabani akubali kwenda nchini Iran kwa mazungumzo

21 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqs

Taarifa kutoka mji mkuu wa Irak, Baghdad, zinasema kwamba rais wa Irak, Jalal Talabani amekubali mualiko wa kushiriki katika mazungumzo mjini Teheran nchini Iran mwishoni mwa wiki, kujadili hali ya sasa nchini Irak. Rais wa Syria, Bashar al-Assad, pia anatarajiwa kuhudhuria mazungumzo hayo. Msemaji wa rais wa Irak amesema mazungumzo hayo yameitishwa kujadili hali ya usalama ilioko nchini Irak na madhara yake katika eneo zima.

Na wakati yakiendelea machafuko ya kidini, waziri wa ulinzi wa Irak ametangaza hali ya kivita nchini humo.