1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Wairaki washangilia ushindi wa timu yao

25 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfP

Milio ya risasi imesikika leo mjini Baghdad huku Wairaki wakisheherekea ushindi wa timu yao ya taifa ya kandanda kufuzu kuingia fainali ya kuwania kombe la Asia. Irak iliishinda Korea Kusini kwa mabao 4-3 kupitia mikwaju ya penalti.

Barabara za mji mkuu Baghdad leo zilijaa mashabiki wa soka waliokuwa wakipeperusha bendera za taifa na kupiga kelele za shangwe.

Televisheni ya taifa imetangaza onyo lililotolewa na makamanda wa jeshi la Irak wakitaka watu wasifyatue risasi angani lakini hakuna aliyelitii onyo hilo.

Ni utamaduni wa Wairak kufyatua risasi angani wakati wa furaha, lakini risasi hizo huua watu zinapoanguka. Watu watatu waliuwawa na wengine takriban 50 kujeruhiwa wakati Irak ilipoishinda Vietnam na kuingia nusu fainali Jumamosi iliyopita.