1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Wakaazi wa Iraq wahitajika kupata msaada wa haraka.

31 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBda

Mashirika ya kutoa misaada yamesema kuwa njaa na magonjwa vinasambaa nchini Iraq, na kwamba karibu theluthi ya wakaazi wa nchi hiyo wanahitaji msaada wa haraka.

Ripoti iliyotolewa na shirika la kutoa misaada la Oxfam na mtandao wa kamati ya uratibu ya mashirika yasiyo ya kiserikali nchini Iraq imesema kuwa ghasia nchini humo zinaficha mzozo huo wa kiutu unaoendelea kukua.

Ripoti hiyo inasema kuwa kuna ongezeko kubwa katika matatizo ya kiutu tangu pale majeshi ya Marekani kuivamia Iraq mwaka 2003, ikiwa ni pamoja na kiwango cha asilimia 30 ya utapia mlo kwa watoto. Shirika la Oxfam liliondoka nchini Iraq pamoja na mashirika mengine kadha ya kutoa misaada miaka minne iliyopita kutokana na kushuka kwa hali ya usalama.