1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Wapiganaji 90 wa al-Qaeda wauwawa.

24 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBou

Jeshi la Marekani limesema kuwa wapiganaji 90 wa kundi la al-Qaeda wameuwawa nchini Iraq katika shambulio kubwa lililofanywa katika jimbo la Diyala siku ya Jumanne.

Majeshi ya Marekani na yale ya Iraq yamesema kuwa yamewakamata wapiganaji wawili waandamizi wa al-Qaeda.

Wengi wa viongozi hao wa wapiganaji wanaaminika kuukimbia mji wa Diyala kabla ya kufanyika operesheni hiyo.

Kwingineko nchini Iraq , wanajeshi saba wa jeshi la Marekani wameuwawa katika mashambulio ya mabomu yalilotegwa kando ya barabara ndani na kuzunguka mji mkuu huo wa Iraq, Baghdad.