1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Waziri Mkuu wa Iraq asema serikali yake inalenga kumaliza ghasia nchini humo.

4 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCV5

Waziri Mkuu wa Iraq, Nuri al-Maliki amesema serikali yake imepania kumaliza ghasia zinazoendelea nchini humo.

Waziri Mkuu Nuri al-Maliki amesema hayo punde baada ya shambulio baya la bomu la kujitolea mhanga lililotokea jana katika soko mjini Baghdad.

Takriban watu mia moja na thelathini waliuawa na wengine mia tatu wakajeruhiwa kwenye shambulio hilo.

Polisi wamesema mtu mmoja aliendesha lori hadi katikati ya soko lililojaa watu na akaripua baruti kiasi ya tani moja kwenye eneo hilo ambalo wakazi wake wengi ni wa madhahebu ya Shia.

Nuri al-Maliki amedai shambulio hilo limetekelezwa na wafuasi wa rais wa zamani, Saddam Hussein, aliyetiwa kitanzi.

Wakati huo huo, mashambulio ya mabomu yametokea mjini Baghdad na kusababisha vifo vya watu watano, wakiwemo askari-polisi wanne na watu kadhaa wakajeruhiwa.