1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD.Helikopta nyingine ya jeshi la Marekani yatunguliwa

7 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUK

Jeshi la Marekani nchini Irak limethibitisha kwamba ndege ya helikopta imetunguliwa katika eneo la kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Baghdad.

Kundi la kigaidi la Al Qaeda nchini Irak limedai kuhusika na shambulio hilo.

Shambulio hilo ni la tano dhidi ya helikopta za jeshi la Marekani katika muda usiopungua wiki mbili.

Walioshuhudia kuanguka kwa helikopta hiyo wameeleza kuwa imeanguka katika eneo linalo kaliwa na Wasunni la Sheikh Amir kaskazini magharibi mwa Baghdad.

Msemaji wa jeshi la Marekani hakutoa maelezo zaidi juu abiria waliokuwa ndani ya helikopta hiyo ingawaje amesema kuwa ina uwezo wa kuwabeba abiria 20.