1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Iran kuhudhuria mkutano wa kimataifa juu ya usalama wa Irak

29 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC5y

Mjumbe wa kimataifa wa Iran bwana Ali Larijan amewasili mjini Baghdad kuanza ziara ya siku tatu nchini Irak. Bwana Larijan aliwasili leo mjini Baghdad bila ya kutangazwa.

Wakati huo huo imethibitishwa kuwa waziri wa mambo ya nje wa Iran bwana Mottaki atahudhuria mkutano wa kimataifa juu ya usalama wa Irak utakaofanyika nchini Misri mapema mwezi mei.