BAGHDAD:Waziri wa Ufaransa Kouchner ziarani Irak
20 Agosti 2007Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa bwana Bernard Kouchner yupo nchini Irak ambapo anafanya ziara ya kwanza ya kiongozi wa ngazi za juu kutoka Ufaransa tokea Irak ivamiwe na majeshi ya nje yaliyoongozwa na Marekani miaka 5 iliyopita.
Baada ya mazungumzo na wenyeji wake waziri Kouchner amesema kuwa ni suluhisho la kisiasa tu, litakalokomesha mauaji nchini Irak.