1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT.Lebanon yadidimia kwenye mzozo wa kisiasa

13 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCt9

Hakuna ishara kwamba mzozo wa kisiasa nchini Lebanon utapata ufumbuzi kwa hivi sasa.

Katika matukio ya hivi punde rais wa Lebanon Emile Lahoud anaeungwa mkono na Syria amemuandikia barua waziri wake mkuu Fouad Siniora kwamba serikali yake si halali tena.

Hatua hiyo imefuatia siku moja tu baada ya mawaziri watano wa makundi ya Hezbollah na Amal walipoamuwa kujiuzulu.

Waziri mkuu Siniora anae elemea upande unao pinga sera za Syria wenye wafuasi wengi katika bunge la Lebanon amekataa kukubali pendekezo la kujiuzulu kwa mawaziri hao hadi sasa.

Maafisa wa Hezbollah wamesema kuwa sasa wanajitayarisha kuitisha maandamano makubwa dhidi ya serikali.

Hali hiyo imezuka baada ya kuvunjika kwa mazungumzo ya wiki moja yaliyolenga kuwapa usemi zaidi serikalini wawakilishi wa makundi yanayounga mkono sera za Syria.