1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BELGRADE : Watafuta muafaka wa Kosovo

11 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBaJ

Wajumbe wa Urusi,Marekani na Umoja wa Ulaya wamekutana na viongozi wa Serbia kuanzisha juhudi za dakika ya mwisho kufikia muafaka juu ya jimbo lililojitenga la Kosovo na dai la uhuru la watu wengi wa kabila la Kialbania wanaoishi jimboni humo.

Ujumbe wa kidiplomasia wa pande hizo tatu umekuwa na mkutano na Waziri Mkuu Vojislav Kostunica na Rais Boris Tadic wa Serbia inayopinga uhuru wa Kosovo.Ujumbe huo wa pande tatu ulianza kulishughulikia suala hilo la Kosovo mwezi uliopita baada ya azimio linaloungwa mkono na mataifa magharibi kuipatia uhuru Kosovo kupingwa katika Umoja wa Mataifa na Urusi kwa niaba ya mshirika wake Serbia.

Wolfgang Ischinger mwanadiplomasia wa Kijerumani ambaye ni mjumbe anayeiwaklisha Umoja wa Ulaya kwenye ujumbe wa kidiplomasia wa pande tatu juu ya mzozo wa Kosovo anasema ingelikuwa hayumo kwenye ujumbe huo wa pande tatu hapo asingelikuwa na imani kwamba inaonekana fursa ya kupatikana kwa maendeleo ni ngumu lakini kwa sababu yuko hapo anaona fursa hiyo iko.

Ujumbe huo wa kidiplomasia wa pande tatu leo unakwenda katika makao makuu ya Umoja wa Kujihami wa Mataifa Magharibi NATO huko Kosovo kwa mazungumzo na viongozi wa Kialbania.