1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEMBA to be transferred to ICC.

Mtullya, Abdu Said2 Julai 2008

Aliekuwa kiongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo yumo njiani kufikishwa mbele ya mahakama ya mjini the Hague,ICC

https://p.dw.com/p/EUY2
Aliekuwa kiongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Picha: AP Photo

BRUSSELS.

Mahakama  ya Ubelgiji imeondoa vipingamizi vyote ili kuwezesha aliyekuwa  kiongozi wa waasi nchini J.K ya  Kongo, Jean Pierre  Bemba kupelekwa mjini  the Hague kujibu mashtaka  ya uhalifu wa  kivita. Mahakama kuu ya Ubelgiji imepinga madai yaliyotolewa na mawakili wa Bemba  kwamba taratibu  za kisheria zilizofuatia ,baada ya kukamatwa  kwake mjini  Brussels  mnamo mwezi  mei hazikuwa sahihi.

Hatua ya kumpeleka Bemba kwenye mahakama ya kimataifa inayopambana na uhalifu ,ICC mjini the   Hague ilikuwa inasubiri uamuzi  wa mahakama.

Uamuzi huo unatarajiwa kutekelezwa karibuni.

Bemba  alikamatwa katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels mwezi mei  kufuatia hati ya kisheria ya  mahakama  ya kimataifa  ya ICC. Anakabiliwa  na mashtaka manne ya uhalifu wa kivita na mawili ya uhalifu dhidi  ya  ubinadamu anayodaiwa  kutenda nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.