1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Madereva wa treni watishia kugoma kazi tena

13 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBJa

Madereva wa treni nchini Ujerumani huenda wakagoma kazi tena siku ya Jumatano,ikiwa shirika la reli la Ujerumani-Deutsche Bahn-hii leo halitotoa pendekezo bora la nyongeza ya mshahara. Kwa mara ya kwanza,Kansela Angela Merkel ameingilia kati mgogoro huo na amezihimiza pande zote mbili kujadiliana upya.Akawaonya kuwa migomo zaidi huenda ikaathiri uchumi wa nchi vibaya sana.