1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Merkel kuboresha ushirikiano baina ya Umoja wa Ulaya na Marekani

2 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCe2

Kufuatia Ujerumani kuchukua uongozi wa Umoja wa Ulaya, kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel anataka kuongeza ushirikiano wa kiuchumi kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani.

Bi Merkel anatarajiwa kulizungumzia swala hili atakapokutana na rais George W Bush wa Marekani mjini Washington baadaye wiki hii.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier ameonya kwamba Bulgaria na Romania bado zinatakiwa kufanya mageuzi makubwa kuweza kufikia viwango vya umoja wa Ulaya.

Steinmeier alisafiri kwenda mjini Bucharest kuadhimisha sherehe za kuikaribisha Romania katika Umoja wa Ulaya. Aliwaambia waandishi wa habari mjini humo kwamba hatua ya Romania kujiunga na Umoja wa Ulaya kunamaliza mgawanyiko wa kihistoria uliokuwepo barani Ulaya.

Steinmeier alisafiri pia kwenda mjini Sofia kuikaribisha Bulgaria katika Umoja wa Ulaya.