1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Mfuko wa watumwa wa kazi wamaliza kazi

12 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsb

Mfuko ulioanzishwa na serikali na viwanda vya Ujerumani miaka sita iliopita kuwalipa fidia watumwa wa kazi umesema umekamilisha kazi yake.

Mfuko huo umegawa euro bilioni 4.4 kwa wahanga milioni 1 na laki saba tokea mwaka 2000.Kila mmoja alijipatia kati ya euro 2,500 na 7,500. Mkuu wa mfuko huo Otto Lambsdorff amesema wengi wa watumwa wa kazi wa zamani walio wakongwe wamepatiwa msaada wa matibabu.

Mpango wa kupunguza wajumbe 27 wa mfuko huo ili kuja kuwa chombo kitakachodhibitiwa na ulimwengu wa shughuli za viwanda kumeelezewa kuwa ni kashfa na chama cha Kijani nchini Ujerumani.Kiongozi mwenza wa chama hicho Reinhard Bütikofer amesema hatua hiyo itawatowa kwenye mfuko huo wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, Ulaya ya mashariki na Israel.

Chama cha sera za mrengo wa shoto cha Left kimesema wafungwa 100,000 wa zamani wa Italia wa wakati wa utawala wa Manazi nchini Ujerumani bado hawakulipwa fidia.

Fedha zilizobakia kwenye mfuko huo zimepangwa kutumiwa kila mwaka katika miradi ya usuluhishi.