1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Mgomo wa treni wagharimu milioni 90

19 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CIlj

Waangalizi wa uchumi wa Ujerumani wanakadiria kwamba mgomo wa madereva wa treni wiki iliopita umeugharimu uchumi hadi euro milioni 90.

Wataalamu katika Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi mjini Berlin wanasema mgomo huo wa masaa 62 kwa usafiri wa treni za mizigo umegharimu euro milioni 80 wakati ule wa abiria umegharimu kati ya euro milioni 5 hadi milioni 10.

Chama cha wafanyakazi madereva wa treni nchini GDL kinadai ongezeko la asimilia 31 ya mshahara kwa madereva wake na kinatishia shirika la reli la taifa Deutsche Bahn kwa migomo zaidi wiki hii venginevyo leo hii linakuja na pendekezo la kuridhisha.