1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Kansela Merkel atoa wito wa kuundwa jeshi la Ulaya kwa awamu

23 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGF

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel ambaye pia ni kiongozi wa Umoja wa Ulaya anatoa wito wa kuundwa jeshi la bara la Ulaya kwa awamu.Bi Merkel aliyehojiwa na gazeti la kila siku la Bild anasema kuwa Kamisheni ya Ulaya ina nafasi kubwa zaidi ya kufafanua majukumu ya jeshi hilo.Hii inatokea ikiwa ni miaka 50 tangu makubaliano ya Rome kufikiwa yaliyopelekea kuundwa kwa Umoja wa Ulaya.

Hata hivyo Kiongozi huyo hataraji kwamba kutaundwa taifa moja la Jamhuri ya Muungano wa Ulaya hivi karibuni.Hayo yanaungwa mkono na Mkuu wa Kamisheni ya Ulaya Jose Manuel Barroso anayesisitiza umuhimu wa kuwa na utajiri wa tamaduni tofauti za mataifa wanachama.

Viongozi hao wanatarajiwa kutia saini makubaliano yanayoelezea hatua zilizopigwa tangu muungano huo kuanzishwa vilevile kutathmini malengo yake.

Suala nyeti linalokabili muungano wa ulaya ni katiba ya Umoja huo baada ya Ufaransa kutupilia mbali rasimu ya katiba hiyo katika kura ya maoni iliyofanywa miaka miwili iliyopita.

Makubaliano hayo yanaazimia kupata suluhu ifikapo mwaka 2009.