1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Ujerumani kupanua uhusiano na bunge jipya la Marekani

9 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuh

Ujerumani imetangaza kwamba inataka kupanua uhusino wake na bunge jipya la Marekani kufuatia ushindi wa chama cha Demokratic katika baraza la wawakilishi.

Karsten Voigt mratibu wa serikali anayehusika na masuala ya uhusiano kati ya Ujerumani na Marekani amesema uchaguzi wa Marekani utasababisha shinikizo zaidi kutoka nchini humo juu ya Ulaya katika kuimarisha shughuli zake Iraq na Afghanstan.

Ujerumani inawanajeshi kiasi 2800 nchini Afghanstan katika kikosi cha umoja wa nchi za kujihami za Magharibi NATO lakini imepinga kupeleka wanajeshi wake huko Iraq.