1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Wafanyikazi wa reli wagoma

2 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmZ

Wafanyikazi wa reli takriban laki moja u nusu wamegoma asubuhi ya leo kwa yapata saa tatu ili kudai nyongeza ya mishahara.Maelefu ya wasafiri hapa Ujerumani wametatizwa na usafiri baada ya hatua hiyo.Kwa mujibu wa msemaji wa shirika la reli la kitaifa Duetsche Bahn huduma zilizoathiriwa ni za safari za kwenda miji ya Frankfurt,Munich,Dortmund,Erfurt,Rostock na Wismar.Migomo ya wafanyikazi wa reli ni nadra sana kutoka hapa Ujerumani.

Vyama vya Transnet na GDBA wanadai nyongeza ya asilimia 7 ya mshahara.

Mgomo mwengine unapangwa kufanyika jumatatu ijayo katika miji ya Hamburg,Karlsruhe na Freiburg.Kampuni ya reli ya Ujerumani Deutsche Bahn kwa upande wake inakubali kutoa nyongeza ya asilimia 2 ifikapo mwaka wa 2008 na 2009 aidha malipo ya euro 300 kwa mpigo mmoja.Pande zoze mbili zilishindwa kuafikiana katika mazungumzo yaliyofanyika jumamosi iliyopita.Kwa mujibu wa kampuni ya reli ya Deutsche Bahn endapo ombi hilo linatekelezwa nafasi alfu 9 za kazi zitakuwa hatarini.