1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beslan, Russia. Kumbukumbu ya mwaka wa tatu yafanyika.

2 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTa

Russia imefanya kumbukumbu ya mwaka wa tatu tangu kutokea kwa mauaji baada ya utekaji nyara katika shule ya Beslan ambapo watu kwa mamia kadha waliuwawa, ikiwa zaidi ya nusu yao walikuwa watoto.

Wapiganaji kutoka jimbo linalotaka kujitenga la Chechnya wakiwa na silaha waliwakamata zaidi ya watoto 1,000 wakiwa na wazazi wao ambao walikuwa wakihudhuria sherehe za ufunguzi wa muhula wa shule katika mji mdogo ulioko katika jimbo la North Ossetia Septemba mwaka 2004.

Zaidi ya wateka nyara 330 waliuwawa katika hatua ya kuzingira shule hiyo , tukio lililomalizika kwa mtafaruku katika jaribio la uokozi.